Page 1 of 12
186
Advances in Social Sciences Research Journal – Vol.7, No.10
Publication Date: January 25, 2021
DOI:10.14738/assrj.81.9604.
Murimi, J., N. (2021) Mwingiliano Wa Utanzu Wa Modern Taarabu- Mipasho Na Maigizo. Advances in Social Sciences Research Journal,
7(10) 186- 197.
Mwingiliano Wa Utanzu Wa Modern Taarabu- Mipasho Na Maigizo
Jackline Njeri Murimi
School of Education, Tom Mboya University College
A constituent College of Maseno University
Ikisiri
Muziki wa taarab umepata mabadiliko makubwa na kusababisha
kuwepo kwa aina mbili kuu za Taarab: Taarab Asili na Modern
Taarab.Utafiti huu ulihakiki mwingiliano tanzu katika Taarab- Mipasho. Malengo ya Makala hii yalikuwa ni kuchanganua miktadha
mbalimbali ya mwingiliano tanzu katika muziki wa Taarab ya Mipasho
na utanzu wa maigizo na kutathmini dhima ya mwingiliano huo katika
muziki wa Taarab ya Mipasho. Makala hii iliongozwa na nadharia ya
mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1960) baada ya
kuizua kutokana na nadharia ya Mikhail Bakhtin ya Usemezano
ambapo imetumika kushughulikia mwingiliano tanzu katika Taarab- Mipasho. Pia nadharia hii imetumika katika kufafanulia uhuru na
ubunifu wa mtunzi wa kuingiza vipengele vipya katika kazi. Utafiti huu
ulichukua muundo wa kimaelezo. Ukusanyaji data ulihusisha
usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini wa nyimbo za Taarab ya
Mipasho ili kupata mistari, vifungu vya maneno na stanza
zilizobainisha mwingiliano tanzu. Sampuli ya utafiti ilikuwa nyimbo 32
za muziki wa Taarab ya Mipasho ambazo ziliteuliwa kumaksudi.
Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulitolewa kwa njia ya maelezo ya
kina yaliyohusisha udondoaji na ufafanuzi wa mistari, vifungu vya
maneno na stanza zenye kudhihirisha mwingiliano tanzu kutoka kwa
data asili. Kutokana na matokeo ya utafiti, mwingilianotanzu mkubwa
ulibainika katika uwasilishaji wa muziki wa Modern Taarab ya
Mipasho uliorejelewa. Utafiti huu unawachochea wahahakiki wengine
wa fasihi simulizi katika kufanya uchunguzi zaidi katika mitindo
mingine ya nyimbo za modern taarab kwa misingi ya nadharia
mbalimbali za fasihi. Aidha, kutokana na utafiti huu, ilitarajiwa kuwa
watafiti wataweza kulinganisha na kulinganua mitindo tofauti ya
taarab. Hatimaye, mtafiti anapendekeza tafiti zaidi zifanywe ili
miongoni mwa mengine, kusuluhisha mgogoro kuhusu taarab ya
mipasho, uwezekano wa kujumuisha nyimbo za taarab miongoni mwa
vipera vya utanzu wa nyimbo katika awamu zote za usomi na uhakiki
wa fasihi simulizi kwani muziki wa taarab na hasa mipasho bado
unahitaji utafiti Zaidi.
Key words: Mwingilianotanzu; Mwingilianomatini; Taarab; Modern Taarab;
mipasho; maigizo